About me

Technology

Friday, May 5, 2017

Kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa

Image result for nguvu za kiume

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

Sababu za Wanaume kuishiwa nguvu za kiume:

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka sababu ya umri. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea ndiyo wanapatwa na tatizo hili zaidi kuliko wanaume wenye umri wa miaka 41 Kushuka chini.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana.
Soma zaidi kuhusu mazoezi kwa kubonyeza hapa => 
Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.
Asilimia 51 mpaka 61 ya wanaume wanaosumbuliwa na kisukari wanapatwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri. Kadharika wagonjwa wa kiharusi na wale waliotekwa na ulevi nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kupatwa kirahisi na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Walevi wengi wa pombe kwa mfano wanakabiliwa na tatizo la uzalishaji mchache wa mbegu za kiume (manii).
Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi wakabaki na majeraha, watu wanaotumia dawa zenye kemikali kiholela bila kushauriwa na wataalamu na wale wanaougua maradhi yanayodhoofisha msukumo wa damu kwenda katika mishipa ya uume.
Pamoja na hayo, tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kutibika kwa watu wa rika zote.
Kabla dakatari hajaanza kukutibu tatizo kupungukiwa nguvu za kiume, atataka kujuwa:
  1. Umri wako
  2. Utendaji wa tendo la ndoa kabla na baada ya kuugua
  3. Afya yako kwa ujumla
  4. Matatizo katika ndoa ikiwa kuna ugomvi wowote n.k
  5. Nini sababu ya wewe kutaka kupona
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kuwa na imani na daktari wako. Kwa kufanya hivi utakuwa umepiga hatua nzuri kelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo lako.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts