New
Mauaji mengine yatokea Rufiji
Rufiji.Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada ya watu wasiojulikana kufika kwake na kutekeleza shambulio hilo.
Marehemu huyo ambaye pia ni mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni baada ya siku tano kuuawa kwa Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa ni mwanachama wa chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani Rufiji, Musa Nyeresa amethibitisha kuuawa kwa mwanachama huyo kwa kupigwa risasi.
No comments:
Post a Comment