About me

Technology

Friday, May 5, 2017

FAHAMU KUHUSU KUVIMBA KWA BANDAMA(Splenomegaly)

Maambukizi na magonjwa mengi kwa muda mrefu husabisha kuvimba kwa bandama(spleen)  ambayo iko kushoto mwa tumbo na hivyo kuharibu utendaji wake wa kazi kama kuondoa vimelea kwenye damu, kutengeneza kinga ya mwili, kuondoa chembe nyekundu zisizo na matumizi mwilini. Ugonjwa huu usababishwa na maambukizi ya virusi, vimelea, bakteria, saratani ya damu, presha, magonjwa ya moyo, ugonjwa sugu wa ini, homa ya ini, upungufu wa damu n.k. Tatizo ili lisipotibiwa husababisaha maambukizi na magonjwa ya mara kwa mara, kuvuja damu na kupasuka kwa bandama.


DALILI
Maumivu makali ya kushoto mwa tumbo yanayoelekea mpaka kwenye bega la kushoto.
Maumivu au kichomi katika kifua tumbo au kibofu vinapojaa.
Maumivu ya mgongo.
Dalili za upungufu wa damu 
Kushiba haraka hasa upande wa kushoto wa tumbo
Maambukizi ya mara kwa mara.
Kutokwa na damu mara kwa mara.
MATIBABU.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya utrasound, MRI au vipimo vya damu na kugundua uwepo wa tatizo ili mara nyini tiba yake huwa ni upasuaji na dawa au chanjo za kupunguza au kujikinga na maambukizi. Pia elimu hutolewa kwa ajili ya kuepuka mambo yanayoongeza presha tumboni kama mazoezi na michezo mikali yenye uwezekano wa kusababisha kuvuja au kupasuka kwa bandama.
Pia wagonjwa wanashauriwa kuvaa mkanda wanapoendesha gari ili kuepuka kupasuka kwa bandama iwapo itatokea ajali.
Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vya asili asa matunda, mboga za majani na viungo ambavyo huongeza kinga ya mwili na kumkinga na magonjwa.
Epuka matumizi ya kahawa, nyama za mafuta, chumvi na sukari nyingi mwilini.
Epuka matumizi ya pombe, madawa, sigara na tumbaku.
Tumia juisi ya mshubiri, machungwa na papai mara mbili kwa siku husaidia kutibu tatizo ili.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts