New
Shamsa Ford avutwa na Nay wa Mitego kwenye ‘Wapo Tour’
Shamsa Ford na Nay wa Mitego
Nay wa Mitego amesema watu wengi huwa wanaamini mkiachana basi ndiyo mwisho wa urafiki lakini kumbe sio hivyo na ndiyo maana hata yeye ameamua kumleta Shamsa Ford kwenye Tour yake ya Wapo.
“Wapo Tour itakuwa ni ya Kipekee sana kwani itakuwa na list ya wasanii wawili watatu hivi wa kunisindikiza, lakini pia atakuwepo Shamsa Ford kwenye Special Appearance pia atakuwa kama MC kwa siku hiyo jukwaani,watu watarajie kuona burudani ya kipekee kabisa“Amesema Nay wa Mitego kwenye mahojiano yake na Bongo Five.
Nay wa Mitego na Shamsa Ford walishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma na baadae kuachana.
‘Wapo Tour’ itaanzia jijini Dar es Salaam tarehe 20 May Mwaka huu pale Dar Live,Mbagala na baadae kuelekea mikoani.
No comments:
Post a Comment