New
Mbunge wa Mtera: Wasiporidhika na Vyeti Watasema Sijatahiriwa Nitatoa Nini...!!? Lusinde
Haya sasa, naona kasi ya vyeti sasa imetua Bungeni,kwa waheshimiwa ambao nao inasemekana hawajakwenda shule.
Zamu hii sakata limetua kwa Mbunge wa Mtera, Mh Livingstone Joseph Lusinde,yeye alisema hivi:-
"Wanaosema sijasoma, nikitoa vyeti wakawa hawajaridhika wakasema pia sijatahiriwa,je nitoe nini?
Haya sasa.
Mheshimiwa Lusinde wakati Wa kampeni za kugombea uraisi Mwaka 2010 walijitokeza wagombea wenza wakatumia hoja ya kuwa Kibajaji hajasoma, wakashawishi wapiga kura wamtake atoe vyeti vyake. Lakini kibajaji Hakuyumbishwa na hizo propaganda akaendelea kupiga kampeni zinazohusu jimbo lake na hatimae wananchi wakamuelewa wakamchagua kwenye kura za maoni na kumpiga chini Mwanasiasa mkongwe Mzee Malecela na baadae wananchi wakachukua wakaweka waaaa!
Siku Moja katika mkutano Wa kampeni baada ya kumaliza kunadi Sera akauliza swali hivi hawa wanaosema sijasoma na wanataka vyeti, Je nikitoa vyeti alafu wasiporidhika wakasema Sijatahiriwa je nitoe nini?
No comments:
Post a Comment